Psalms 144

Mfalme Amshukuru Mungu Kwa Ushindi

(Zaburi Ya Daudi)


1 aSifa ni kwa Bwana Mwamba wangu,
aifundishaye mikono yangu vita,
na vidole vyangu kupigana.

2 bYeye ni Mungu wangu wa upendo na boma langu,
ngome yangu na mwokozi wangu,
ngao yangu ninayemkimbilia,
ambaye huwatiisha mataifa chini yangu.


3 cEe Bwana, mwanadamu ni nini hata umjali,
Binadamu ni nini hata umfikirie?

4 dMwanadamu ni kama pumzi,
siku zake ni kama kivuli kinachopita.


5 eEe Bwana, pasua mbingu zako, ushuke,
gusa milima ili itoe moshi.

6 fPeleka umeme uwatawanye adui,
lenga mishale yako uwashinde.

7 gNyoosha mkono wako kutoka juu,
nikomboe na kuniokoa
kutoka maji makuu,
kutoka mikononi mwa wageni

8 hambao vinywa vyao vimejaa uongo,
na mikono yao ya kuume ni midanganyifu.


9 iEe Mungu, nitakuimbia wimbo mpya,
kwa zeze yenye nyuzi kumi nitakuimbia,

10 jkwa Yule awapaye wafalme ushindi,
ambaye humwokoa Daudi, mtumishi wake kutokana na upanga hatari.


11 kNikomboe na uniokoe
kutoka mikononi mwa wageni
ambao vinywa vyao vimejaa uongo,
na mikono yao ya kuume ni midanganyifu.


12 lKisha wana wetu wakati wa ujana wao
watakuwa kama mimea iliyotunzwa vizuri,
binti zetu watakuwa kama nguzo zilizoviringwa
kurembesha jumba la kifalme.

13 mGhala zetu zitajazwa
aina zote za mahitaji.
Kondoo zetu watazaa kwa maelfu,
kwa makumi ya maelfu katika mashamba yetu;

14 nmaksai wetu watakokota
mizigo mizito.
Hakutakuwa na kubomoka kuta,
hakuna kuchukuliwa mateka,
wala kilio cha taabu
katika barabara zetu.


15 oHeri watu ambao hili ni kweli;
heri wale ambao Bwana ni Mungu wao.
Copyright information for SwhKC